Baraza la Wilaya la Chalinze, likiwa chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, limeandaa mtihani wa kujiandaa kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika wilaya. Mitihani hii inajulikana kama “FORM FOUR PRE – MOCK EXAMINATION 2024” na itaanza tarehe 15 Aprili 2024
Ratiba ya mitihani unaweza kuipata kwa kubonyeza link download FORM 4 PRE – MOCK EXAMINATION TIMETABLE 2024
Lengo la Mtihani
Lengo kuu la mtihani huu ni kuwapa wanafunzi wa kidato cha nne fursa ya kujaribu ujuzi wao na kujiandaa vyema kwa mtihani halisi wa kidato cha nne unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu. Mtihani huu utasaidia wanafunzi kutambua maeneo yao dhaifu na yenye nguvu, na pia kuwapa mwongozo wa jinsi ya kuboresha ufaulu wao.
Ratiba ya mitihani unaweza kuipata kwa kubonyeza link download FORM 4 PRE – MOCK EXAMINATION TIMETABLE 2024
Tunaamini mitihani hii itakuwa na manufaa makubwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika Wilaya ya Chalinze na kuwawezesha kufanikiwa vyema katika mtihani halisi wa kidato cha nne.
Asante.
Good luck kwa watahiniwa wote mungu awaongoze na awe nanyi kwa kila hatua muipigayo kwenye masomo yenu
Mtaani kugumu wadogo zangu